Jeshi la Polisi Dar lilivyozikusanya Mil 577 za wakosaji Barabarani

Polisi Kanda maalum Dar es salaam kupitia kitengo cha usalama barabarani wametoa taarifa ya makosa ya barabarani kuanzia March 07 2016 hadi March 18 2016 kuwa wamefanikiwa kukamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani na jumla ya Tsh Milioni 577.8 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa muda wa siku 11.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema…..>>>‘madereva wametakiwa kuwa waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku’
Post a Comment