Mtanzania mfungwa ampigia simu Millard Ayo akiwa ndani ya gereza Macau China..(+Audio)

Mtanzania aliyefungwa gerezani China ambaye jina lake limehifadhiwa, kutoka ndani ya gereza alilofungwa huko Macau China amempigia simu Mtangazaji na Mwandishi wa habari Millard Ayo na kuelezea maisha ya gerezani, jinsi alivyokamatwa, Watanzania wenzake na mengine
Mtanzania huyu aliyefungwa toka mwaka 2007 ameanza kwa kuhadithia alivyokamatwa na kusema ‘Ilikuwa mambo ya madawa, mimi nilikuwa nimetoka Dubai kuja China, jamaa wakaingia katika hoteli na wakatukamata jumla tulikuwa watu nane tukakamatwa wote‘
‘Ujue nchi hii mambo ya madawa wanapiga vita mno, kesi za madawa zina adhabu ya miaka mingi kuliko kesi nyingine yoyote, kama mimi nimefungwa miaka kumi na miezi sita, nilifungwa nikiwa na miaka kama 26, nilianza kufanya biashara ya dawa za kulevya nikiwa na miaka kama 18, niko gereza moja na Jackie Cliff”
Kwenye sentensi nyingine, Mfungwa huyu amezungumzia siku ya kwanza alipomuona Jackie Cliff gerezani na pia Watanzania wengine waliofungwa kwenye hilo gereza, kazi wanazofanya na kulipwa mshahara japo wapo gerezani na mengine, ukitaka kuipata full stori ya Mfungwa huyu bonyeza play kwenye hii video hapa chini umskie akihadithia kila kitu….
Post a Comment