Header Ads

ad

Filamu nyingine ya Avatar kuongezwa hadi mwaka 2023

150623095312_a_scene_in_avatar_624x351_rexfeatures_nocredit

Muongozaji wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa 2023.
Alikuwa tayari amethibitisha kwamba filamu tatu zaidi zingetolewa lakini amefichua kwamba kuna mambo mengi sana ya kuelezwa kwenye hadithi hiyo na makala zijazo tatu hazitoshi.
Kote duniani, Avatar inasalia kuwa filamu iliyofanikiwa zaidi katika historia. Filamu hiyo imezoa $2.7bn tangu kutolewa wake 2009. Filamu ijayo ya Avatar itatoka 2018, na hizo nyingine 2020, 2022 na 2023.