Barcelona waanza kuchoshwa na starehe za Neymar, safari yake PSG yanukia
Tetesi zinazidi kutanda kwamba Neymar anakwenda PSG, mwaka 2000 wakati Luis Figo anaenda Real Madrid ulikuwa usajili gumzo sana na sasa Barcelona wanaonekana kutaka kufanya usajili gumzo mwingine.
Barcelona wanamuhitaji sana Neymar lakini taarifa zinaeleza kwamba wameshaanza kuchoshwa na tabia zake za kula bata sana ambazo zinampelekea kutokuwa fiti mara nyingi na kuumia umia.
Kama unakumbuka mchezaji mwingine wa zamani wa Barca na Brazil mshambuliaji Ronaldinho Gaucho alilazimika kuondoka Ulaya kutokana na kiwango kuporomomoka ghafla hali iliyochangiwa na starehe zilizopitiliza na Barcelona wana hofu hilo linatokea kwa Neymar pia.
Katika siku za usoni Neymar amekuwa akipiga picha nyingi sana batani na tofauti na wenzake hata katika msimu wakati ligi inaendelea alikuwa akionekana akila bata viwanjani kama kawaida.
Usiku ambao Barca waliitoa PSG baada ya mechi Neymar alienda kula bata refu na muendesha langalanga Lewis Hamilton, baada ya kutoka batani kesho yake akaumia mazoezi na akakosa mchezo uliofuata wa ligi zidi ya Deportivo ambapo Barca walikufa.
Pia taarifa zinadai kwa miaka mitatu mfululizo Neymar amekuwa akikosa michezo inayochezwa siku za karibu na birthday ya dada yake aitwaye Rafaella kwani mara zote huhudhuria, na pia urafiki wake na Justin Bieber unamfanya naye ale bata kama msanii.
Ofa ya Nasser El Khaifi tajiri wa PSG ya £222m inaweza kuwashawishi Barca kumuuza tu na taarifa zinasema viongozi wa klabu hiyo wameshaanza kujadili juu ya deal hilo la Neymar kwenda PSG.
Pamoja na sababu zote hizo lakini bado pia mshambuliaji huyo mwenyewe hataki kucheza pembeni ya Messi na Suarez kwani inaaminika uwepo wa nyota hao wawili unamzuia Neymar kuwa mchezaji bora wa dunia.
Neymar anahitaji sehemu ambayo atakuwa huru, anahitaji sehemu ambapo timu itatengenezwa kupitia yeye na yeye atakuwa mfalme na kwenda PSG ndio mahala sahihi kwake

Post a Comment