Header Ads

ad

Kama ulipitwa na vituko vya 16 bora ya Ndondo Cup Kauzu FC vs Stimtosha

Hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup 2017 inaendelea katika Uwanja wa Kinesi uliopo Victor Wanyama Street ambapo July 20, 2017 tulishuhudia safari ya Kauzu FC kwenye michuano hiyo ikifika mwisho baada ya kufungwa kwa penalti 4-2 dhidi ya Stimtosha.
Mgeni Rasmi katika mchezo wa Kauzu FC vs Stimtosha, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
Mchezo huo uliingia hatua ya penalti baada ya sare ya 1-1 katika muda wa kawaida ambapo Kauzu FC wakiwa wa mwanzo kupata bao la kuongoza lililofungwa na Nahodha Geofrey Taita dakika ya 22 kabla ya Ally Kagawa kuisawazishia Stimtosha dakika ya 72.
Mgeni Rasmi Ridhiwani Kikwete akikabidhi zawadi kwa Stimtosha FC baada ya kuishinda Kauzu FC kwenye mchezo wa Ndondo Cup