Header Ads

ad

Aliyesema ‘Mume Bwege’ wa Bushoke na ‘She Got A Gwan’ Ngwea nimeandika mimi, ameninukuu vibaya – Soggy Doggy

Msanii mkongwe wa muziki, Soggy Doggy amekanusha taarifa zilizozangaa katika mitandao ya kijamii kuwa ndiye aliyeandika wimbo wa Bushoke ‘Mume bwege’ pamoja na ‘She Got A Gwan’ ya Ngwea.
soggy-2
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Soggy Doggy alisema kuwa hakusema kuwa yeye ndiye aliyeandika kazi hizo bali alisema yeye ndiye aliyesaidia kuziandaa katika production wakati yupo kwa P Funk Majani.
“Hawa jamaa wanataka kunigombanisha na wadogo zangu, mimi sijasema hivyo, wameninukuu vibaya,” alisema Soggy.
“Mimi nilikuwa Times FM nafanyiwa interview na Monalisa na sikusema hivyo hata wao ukiwauliza watasema. Mimi nilitengeneza beat ya She got a gwan ya Ngwea, Mume Bwege ya Bushoke na nyingine, na baadhi ya vitu vingine walimalizia akina P-Funk. Wasanii ambao niliwahi kuwaandikia nyimbo ni Suma G, lakini sijawahi kumuandikia Bushoke, hao jamaa wanataka kunikosanisha na watu wangu,” aliongeza Soggy.
Mtandao huo