Header Ads

ad

Tundaman apata ajali mbaya ya gari, aliyekuwa akiendesha apoteza maisha

Muimbaji wa Tip Top Connection, Tundaman, amepata ajali mbaya ya gari Jumapili hii.
Tunda
Tunda
Ajali hiyo imetokea katika eneo liitwalo Idetelo, Nyololo katika mji wa Makambako wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Aurion
12917927_1165743726791687_492381393_n
Gari aliyokuwa amepanda Tundaman baada ya ajali

12917927_1165743726791687_492381393_n
Aliyekuwa dereva wa gari hilo amepoteza maisha na mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Meneja wa kundi hilo, Babutale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
“Nimepokea simu nyingi za kuulizwa hali ya msanii wangu @tundamantz mungu mkubwa ametoka salama ingawa wamepata mtihani mkubwa wa kumpoteza dereva aliyekua anaendesha gari yao amefariki Hapo Hapo. Kazi yake mola aina makosa,” ameandika Tale kwenye Instagram.